Indonesia imewaua wauzaji wanane wa mihadarati baada ya kutoa hukumu ya kifo dhidi yao.
Hukumu
hiyo imetekelezwa na kikosi maalum cha kuwapiga wafungwa risasi, licha
ya mwito kutoka kwa mataifa ya dunia ya kuwahurumia watu hao.Kuuwawa kwa mfungwa wa tisa, raia wa Ufilipino, Mary Jane Veloso, kumecheleweshwa baada ya mwanamke mmoja kujiwasilisha kwa polisi Nchini Ufilipino, akisema kuwa ndiye aliyemhadaa mfungwa huyo mwanamke mwenzake, kupeleka dawa za kulevya hadi Indonesia.
Source:BBC
0 comments:
Post a Comment