Watu 10 wamefariki dunia kwa ajali iliyohusisha magari matatu katika
eneo la Mkata kijiji cha Mbweni wilayani Handeni Mkoani Tanga majira ya
saa 5 asubuhi ya leo.
Akizungumza na Mwandishi wetu Kamanda
wa kikosi cha usalama barabara mkoa wa Tanga amesema kuwa ajali hiyo
imehusisha mabasi mawili ya abiria na gari dogo katika barabara ya Dar
es salaa kwenda Tanga na Arusha.
Kwa mujibu wa Kamanda, gari dogo ilikuwa likitaka kulipita lori lililokua
mbele yake na ndipo ilipogongana uso kwa uso na basi la Ratco
lililokuwa likitokea Tanga kwenda Dar es salaam.
Baada ya Basi la Ratco kugonganana na gari dogo, lilipoteza mwelekeo na kugongana tena uso kwa uso na basi la Ngolika lililokuwa likitokea Dar es salaam kwenda Arusha.
Aidha kamanda huyo amesema kuwa kati ya watu 10 waliofariki dunia wanaume watano wakiwemo dereva wa gari dogo na dereva wa basi la Ngorika pamoja na wanawake watano wakiwemo watoto wawili.
Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi

0 comments:
Post a Comment