Nuh Mziwanda Anusurika Kupigwa Chupa na Shilole ambaye ni Mpenzi Wake.....Hili ni tukio la Pili
Staa wa Bongo Fleva na Bongo Movie,Shilole amedaiwa kutaka kumpiga tena mpenzi wake ambaye pia ni msanii Nuh Mziwanda kwa chupa hivi karibuni wakiwa kwenye sherehe ya kuzaliwa meneja wa msanii Kajala,aitwaye Lamata iliyofanyika pande za Samaki Samaki,Posta,jijini Dar.
Katika tukio hilo habari zinasema kuwa Shilole alikuwa
amelewa sana na kwamba walikuwa wamekaa sehemu tofauti na Nuh
Mziwanda,ghafla sehemu aliyokuwa amekaa Nuh na wasanii wengine ilirushwa
chupa ambayo ilikuwa ikimlenga msanii huyo bahati nzuri aliikwepa
ikampiga jamaa mmoja lakini haikumjeruhi.
Baada ya tukio hilo ilibidi baadhi ya wasanii wamuijie juu
Shilole na kumuuliza kwanini alitaka kumpasua Nuh kwa chupa,Shilole
alianzisha ugomvi na kuzua tafrani kwenye sherehe hiyo baadaye aliamua
kukaa pembeni peke yake na kuanza kulia.
‘’Yaani unaambiwa kama ile chupa ingempata Nuh sasa
hivi tungekuwa tunaongea mengine alikuwa anamjeruhi vibaya sana kiukweli
alileta fujo sana kwenye ile sherehe,"alisema mmoja ya watu walikuwa kwenye sherehe hiyo.
Baada ya hapo msanii Quick Racka alimfuata Shilole na
kumwambia kuwa kumbe akilia anakuwa mbaya ndipo aliamka na kumrushia
chupa ambayo kwa bahati nzuri Quick Racka naye aliikwepa ikapasuka
chini.
Hata hivyo Soudy Brown kupitia Uheard alipompigia simu
Shilole kumsomea mashtaka hayo alimwambia asimsumbue kwani kwa muda huo
alikuwa amelala.
Shilole amekuwa akimpiga na kumdhalilisha mpenzi wake Nuh
Mziwanda kwa kumpiga hadharani mara kwa mara ambapo miezi ya hivi
karibuni alimpiga vibao kwenye tamasha moja lililofanyika pande za
viwanja vya Leaders na baadaye kumuomba msamaha mpenzi wake kupitia
vyombo vya habari na kuahidi kutompiga tena.
0 comments:
Post a Comment