Mama Maria Nyerere ambaye ni mjane wa mke wa Rais wa kwanza wa Tanzania, hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, jana jioni alizungumza na kituo cha runinga cha Taifa, TBC na kukanusha uvumi ulioenezwa katika mitandao ya kijamii kuwa ameaga dunia.
Akizungumza na mtangazaji, Mama Nyerere alimuuliza, "ukiniangalia
unanionaje?" ambapo mtangazaji alimjibu, "nakuona mzima!" huku
wakitabasamu.
Mama Maria alisema huu ni mwaka wa uchauguzi, hivyo mambo haya ya uzushi si ya ajabu.
Kabla ya uvumi wa kizushi kuhusu Mama Maria, juzi kupitia WhatsApp
ulikuwa ukitumwa ujumbe mwingine wa kumzushia kifo Reginald Mengi,
Mwenyekiti wa makampuni ya IPP.
0 comments:
Post a Comment