Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Monday, March 9, 2015

Hakimu Afikishwa Mahakamani Kwa Utekaji, Wizi na Kumpiga Picha Za UCHI Mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi akimtuhumu Kutembea na Mumewe


Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo ya Somanda Wilayani bariadi Janeth Mazigi (28) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Bariadi kwa makosa manne (4) aliyoyatenda dhidi ya mtumishi wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi kwa kile kinachosadikiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Hakimu huyo inadaiwa kuwa alitumia wadhifa alionao kumteka mtumishi huyo (jina linahifadhiwa) na kumnyanyasa kijinsia kinyume na sheria ya kanuni ya Adhabu sura ya 16.

Akisomewa mashtaka hayo na Wakili wa Serikali Mfawidhi Mkoani hapa Yamiko Mlekano mbele ya hakimu Mfawithi mahakama ya wilaya Bariadi Aidan Mwilapwa wakili huyo alisema kuwa mshitakiwa anatuhumiwa kwa kosa la  wizi, utekeji, unyanyasaji, pamoja na kukutwa na picha utupu.

Mlekano aliieleza mahakama kuwa mnamo tarehe 3/03/2015 mshtakiwa pamoja na askari polisi wa kike walimteka Mtumishi huyo ofisini kwake kinyume na matakwa yake na kumpeleka nyumbani kwa mshitakiwa Kidinda Bariadi Mjini kinyume na kifungu namba 133 cha kanuni ya adhabu sura ya 16.

Kosa la pili la unyanyasaji wa kijinsia, ilidaiwa kuwa katika tarehe hiyo hiyo majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwa Mshtakiwa , alimpiga picha za utupu mtumishi huyo kwa kutumia simu yake kwa lengo la kumdhalilisha na kumtolea maneno ya kashfa.

Kosa la tatu kukutwa na picha za udhalilishaji, mshitakiwa ilidaiwa terehe hiyo hiyo majira ya saa 3 asubuhi nyumbani kwa mshitakiwa alikutwa na picha za utupu zilizokuwa katika simu yake alizokuwa amempiga mtumishi huyo akiwa uchi kwa lengo za kuzituma katika mitandao ya kijamii ili kumdhalilisha kinyume na sheria na kanuni ya adhabu.

Kosa la nne ambalo ni wizi, ilidaiwa mshitakiwa alimnyanganya mtumishi huyo kiasi cha pesa taslimu Tsh 50,000, power bank, chaji, airphone, simu mbili za aina ya Son na Tecno vyote hivyo vikiwa na thamani ya Sh Mil 1,405,000.

Hata hivyo mshitakiwa alikana makosa hayo, ambapo aliachiwa baada ya kupata dhamana, huku hakimu wa mahakama hiyo akiahirisha kesi hadi tarehe 2/04/2015.

Hata hivyo mshitakiwa huyo wakati anatenda makosa hayo alishirikiana na askari polisi kituo cha polisi Bariadi, ambaye hakuweza kupatikana jina lake, huku taarifa zikisema kuwa askari huyo bado anashugulikiwa na mamlaka zilizoko chini yake kijeshi.

Mshtakiwa anadaiwa kutenda makosa hayo nyumbani kwake huko Kidinda na kwamba chanzo kinasadikiwa ni wivu wa mapenzi ambao ulipelekea kumtuhumu mtumishi huyo kuwa anatembea na mume wake.

0 comments: