Mazishi
ya Mbunge wa Mbinga Magharibi na mkurugenzi wa TOT Kapten John Komba
yatafanyika Mbinga kesho (Jumanne) huku wakazi wa jiji la Dar es
Salaam wakitarajiwa kuuga mwili wake leo Jumatatu katika viwanja vya
Karimjee.
Komba alifariki ghafla Jumamosi mchana katika hospitali ya TMJ ya jijini Dar es Salaam.
Katibu
Mipango wa TOT Gasper Tumaini amesema kuwa mwili wa Kapten
Komba utaanza kuagwa hapo Karimjee saa nne za asubuhi na kuendelea kabla
ya kusafirishwa kwenda kwao Mbinga tayari kwa mazishi yatakayofanyika
Jumanne.
0 comments:
Post a Comment