Kiungo wa kati wa Sporting Lisbon William Carvalho anayelengwa na Arsenal
.
Arsenal wanadaiwa kumfukuzia William Carvalho.Kiungo
huyo wa kati wa Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 22 anaweza kucheza
katika safu ya kati ya ulinzi na amekuwa akilengwa na Gunners kwa mda
mrefu licha ya kuwa na bei ghali.
Kilabu ya Sporting Lisbon
inataka kitita cha pauni millioni 30 ,lakini kulingana na gazeti la
daily mail nchini Uingereza kocha wa Arsenal Arsene Wenger anapanga
kulipa pauni 25.5.
Vilevile Wenger ameripotiwa kutaka kumchukua kiungo wa kati wa Newcastle Moussa Sissoko kwa kitita cha pauni millioni 9.
Moussa Sissoko wa Newcastle
Wakati huohuo meneja wa
Manchester City Manuel Pelegrini anatarajiwa kumununua mshambuliaji wa
Swansea Wilfried Bonny ili kuchukua mahala pake Sergio Aguero ambaye ana
jereha la mguu.
Gazeti la Daily Telegraph limeripoti kuwa
Manchester City pia inajiandaa kumnunua mshambuliaji huyo kwa takriban
pauni millioni 30.
Hatahivyo kulingana na The Times ,Chelsea pia inamtaka mshambuliaji huyo.
0 comments:
Post a Comment