Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe |
Siku chache baada ya Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe kumfuta kazi makamu wake Joyce Mujuru na mawaziri wanane, kiongozi huyo amewateua na kuwaapisha shaksia wengine kujaza nafasi hizo za uwaziri baada ya kufanya mabadiliko machache kwenye baraza la Mawaziri.
Emmerson Mnangagwa ambaye siku chache zilizopita aliteuliwa kuwa Makamu wa Kwanza wa Rais ataendelea pia kushikilia wadhifa wake wa Waziri wa Sheria. Baadhi ya mawaziri waliobadilishwa ni pamoja na Oppah Muchinguri ambaye ametolewa kwenye Wizara ya Wanawake na Maendeleo ya Jamii na kupelekwa Wizara ya Elimu ya Juu.
Rais Mugabe alimfuta kazi makamu wake Joyce Mujuru na mawaziri 8 siku ya Jumanne iliyopita baada ya kuwatuhumu kuwa walikuwa wakipanga njama ya kumuua. Hatima ya Mujuru na wenzake waliotimuliwa bado haijabainika.
0 comments:
Post a Comment