MAYWEATHER AKIWA NA RAPA HUYO PAMOJA NA MKEWE. |
Bondia Floyd Mayweather ameshindwa kumshawishi rapa Earl Hayes asimuue mkewe.
Rapa huyo alimpigia simu Mayweather kutumia mfumo wa FaceTime unaowawezesha wanaowasiliana kuonana na kumueleza anataka kumuua mkewe Stephanie Moseley.
HAYES |
Mayweather alianza kazi ya kumshawishi asifanye hivyo, lakini huku Mayweather akishuhudia kupitia simu, rapa huyo alimmaliza mkewe.
Baada ya hapo alizungumza na Mayweather kabla ya yeye pia kujimaliza.
Jirani wa eneo high-end jijini Los Angeles waliwapigia simu polisi.
Polisi walifika eneo la tukio na kulazimika kuvunja mlango na kukuta wote wakiwa wamefariki dunia kwani baada ya kummaliza mkewe, rapa huyo naye alijitwanga risasi.
Mkewe alikuwa mmoja wa wacheza shoo na waimbaji kwa kushirikiana na wasanii mbalimbali.
0 comments:
Post a Comment