Muziki,Habari motomoto,MICHEZO,Maajabu,Picha Picha na mambo mengine mengi hapa ndani ya KALI ZA DJ YEYO

nongona

tangazo eligod

tangazo eligod

About the Author

CHECK me!!!!

CHECK me!!!!

Tuesday, December 16, 2014

Dirisha la usajili lafugwa Tanzania


   
Simba na Yanga zimeshamaliza usajili jana usiku.
Usajili wa wachezaji kwa dirisha dogo nchi Tanzania kwa msimu wa mwaka 2014/2015 umefugwa rasmi jana usiku kwa vigogo wa soka Simba, Yanga pamoja na Azam kusajili nyota wengi wa kigeni
Simba Sc yenye maskani yake mtaa wa msimbazi wamefanya usajili wa wachezaji Hassan Kessy toka Mtibwa, Dan Sserunkuma ,Simon Sserunkuma, na Beki Juuko Murushid toka Uganda na kukamilisha idadi ya wachezaji watano toka Uganda akiwemo Joseph Owino na mshambuliaji Emmanuel Okwi.


Kwa upande wa Yanga wamefanya marekebisho ya kikosi chao kwa kuwasajili Dany Mrwanda ,Kpah Sherman toka Aries Fc na Amisi Tambwe toka Simba Sc.
Huku mabigwa watetezi Azam wakiwasajili beki Serge Wawa Pascal kutoka Ivory Coast, aliyekuwa anacheza El Merreikh ya Sudan na Amri Kiemba aliyekuwa Simba SC, na winga Brian Majwega toka klabu ya Kcca.


Vinara wa ligi Mtibwa Sugar wamewaongeza kiungo mzoefu Henry Joseph Shindika, na Abdul Jeba toka klabu ya Chuoni ya Zanzibar.


Timu nyingine zimefanya pia usajili wa kuboresha vikosi vya kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa kuu ya Tanzania bara maarufu kama VPL.


Jumla ya wachezaji 15 wa kigeni wameombewa ITC ili kuweza kuzitumikia timu zao kabla ya raundi ya pili kuanza.


Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya chama cha mpira Tanzanian(TFF) inatarajia kukutana hivi karibuni kwa ajili ya kupitia usajili wa wachezaji wote walioombewa katika dirisha dogo wakiwemo wale wa mkopo

0 comments: