MSANII wa muziki wa kizazi kipya bongo, Dayna, amesema baada
ya ngoma yake ya ‘Nivute kwako’, kufanya vizuri sasa anatarajia
kuachia ngoma mpya inayokwenda kwa jina la ‘Nenda
Nenda’, na sasa kasimama mwenyewe ili kuwaonesha mashabiki uwezo
wake zaidi.
Dayna akizungumza katika the GAME show na DJ YEYO,amesema kwa ufupi ngoma inahusu
mapenzi, kwamba alikuwa katika mahusiano lakini mpenzi wake huyo mara
nyingi alikuwa anakosea na alipomsihi abadilike hakuweza kwenda kule
anakokutana ndipo alipoamua kumuacha na kumwambia ‘Nenda Nenda’. kwani
anaamini bado hajampata aliyeandikiwa na mungu.
“Ndani ya ngoma hii
nimekuwa na huzuni sana kwani mpenzi wangu hakuwa yule niliyeandikiwa na
mungu hivyo ananifanyia mambo mengi ambayo hayana msingi, hivyo nawaomba
mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwani siku si nyingi mzigo unakuja
na nimesimama mwenyewe mwanzo mwisho,” alisema.
Hata hivyo ameongeza kuwa kwa upande wake ameamua kubandilika
kwani wanawake wengi wanaofanya muziki huo wanafanna hivyo yenye ameamua
kwenda tofauti kidogo kuanzia kwenye mavazi, uchezaji, na hata katika
upande wa kutengeneza mwili na uwe katika hali ya mazoezi muda wote.
Pia alisema kuwa anafanya mchakato wa kuzungumza na baadhi ya
wadau kwa ajili ya kufanya show za nje kwani tangu amekuwa kwenye muziki
huo hajawahi kusafiri na nje ya nchi zaidi ya kupiga show za hapa hapa.
Hata
hivyo alipoulizwa kuhusiana na soko je muziki wake unafanya vizuri
sokoni, alijibu kwa upande wake anashukuru mungu pamoja na mashabiki wake
kwani kila ngoma anayoachia mashabiki wanaipokea vizuri.
0 comments:
Post a Comment