China ni
miongoni mwa Mataifa makubwa duniani ambapo uchumi wake unazidi kukua
pamoja na miundombinu yake, ndiyo nchi pekee inayoongoza kwa miundombinu
ya madaraja yaliyovunja rekodi kwa ubora duniani, hivi karibuni
imeripotiwa kuzunduliwa kwa daraja lililotengenezwa kwa vioo.
Daraja la
kioo ambalo limeelezwa kuwa liko juu zaidi limezinduliwa hivi karibuni
nchini China ambapo lina urefu wa zaidi ya futi 1400, upana wa futi 20
na karibu futi 1000 kutoka kwenye ardhi na imeripotiwa kuwa kioo chake
ni imara zaidi mara 25 zaidi ya kioo cha dirisha.
Daraja
hilo la wapita kwa miguu lijulikanalo kwa jina la daraja la Zhangjiajie
limezinduliwa July mwaka huu ambapo lina uwezo wa kuchukua watu hadi 800
kwa wakati mmoja. Imeelezwa kuwa daraja hilo limekuwa likitumika kwa shughuli mbalimbali za kiutalii.
0 comments:
Post a Comment